Friday, 16 January 2015

VANESA MDEE ACHAGULIWA KUWA BALOZI WA SAMSUNG TANZANIA


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Ya Samsung Tanzania Mike Seo akibadilishana Mkataba na Msanii Vanessa Mdee pamoja na Meneja wake Michele Baldini.

Vanessa Mdee akiwa katika picha ya Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania Mike Seo, Silvester Manyara Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania pamoja na Meneja wa Vanessa Mdee Michele Baldini

Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Tanzania akimkabidhi simu msanii wa Muziki Tanzania Vanessa Mdee

Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Tanzania akitia Saini Mkataba wa makubaliano baina yao na Msanii Vanessa Mdee

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania akiongea na wanahabari

Vannessa Mdee akiongea na wanahabari
Dar es Salaam, 16 Januari 2015; Kampuni ya kielektroniki ya Samsung kwa mara ya kwanza imehusisha kampuni hiyo na msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania. Leo hii, Kampuni namba moja duniani inayoongoza kwa technolojia ya hali ya juu, Samsung wanayo furaha kumtangaza balozi wao mpya mwanamziki nyota, na mtangazaji wa Televisheni na radio Vanessa Mdee.
Katika mkutano na wanahabari ulilofanyika hoteli, ya Hyatt Regency, iliyoko mjini Dar es Salaam iliohusisha kusaini kwa mkataba baina ya Vannesa Mdee na uongozi wa kampuni ya Samsung ni ishara tosha ya makubaliano rasmi kati ya Kampuni ya Samsung na msanii huyo. Kitendo hicho kilihashiria mwanzo wa kazi mpya kwa Vanessa Mdee kama mwakilishi wa kampuni ya Samsung nchini Tanzania.
Akiwa kama balozi wa kampuni ya Samsung, Vanessa atakuwa kiungo muhimu katika muonekano na uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung, Mheshimiwa Mike Seo alisema kuwa, "kwa kutambua ongezeko la uhitaji wa simu za kisasa kwa soko la kati nchini Tanzania ni bora kuwasiliana na wateja wetu kupitia mtu ambaye amebeba sifa zinazoendana na vifaa vyetu na soko letu. Anaongeza kuwa "Tunafuraha sana kutangaza ushirikiano wetu na Vanessa Mdee akiwa kama Balozi wetu mpya nchini Tanzania. Akiwa kama mwanamziki nyota na mchangiaji chanya kwa wananchi wa Tanzania. Vanessa anawakilishi vijana wa kisasa wa Tanzania na ni mtu ambaye kampuni ya Samsung inaweza kufanya naye kazi hivyo basi tunafuraha kubwa kuwa na mtu kama huyu kuwakilisha bidhaa zetu. "
Vanessa Mdee ambaye aliongozana na menejimenti yake kwenye mkutano huo, alielezea juu ya furaha yake kwa kuwa sehemu ya kampuni ya Samsung, alisema "Samsung ni kampuni kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya kielektroniki ulimwengu, huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015 utakavokuwa wa mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung. Binafsi, natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi. "


Kuhusu ya Samsung .


Samsung Electronics Co., Ltd. Ni kampuni gwiji la vifaa vya kieletroniki linalofungua milango kwa watu duniani. Kupitia uvumbuzi na ugunduzi tunabadilisha ulimwengu wa TV, simu za kisasa, tablets, kompyuta, kamera, printa na vifaa vya nyumbani. Na tumetoa jira kwa zaidi ya watu 286,000 katika nchi mbali mbali duniani na makadirio ya mapato yapatayo dola bilioni 216.7. Tembele tovuti yetu kupata maelezo zaid kuhusu kampeni yetu www.samsung.com.


Kuhusu Vanessa.

Juu ya mwendo wa kazi zake, muimbaji wa Tanzania, mtunzi wa nyimbo, na mwanamuziki nyota Vanessa ametoa nyimbo tano ikiwa ni pamoja na Closer, Hawajui, Come Over, Wave Clap dance na Siri, pia ameshirikishwa katika nyimbo kama Me and you na Ommy Dimples, Money na AY, Monifere na Gosy B, Bashasha na Bob Junior na Nisamehe na Angle. Vanessa alishinda tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tuzo nne za Kill Music Awards na moja ya Afrika all Music Award. Amekuwa akijihusisha na kampeni mbalimbali kama vile Staying Alive Foundation Project, kampeni ya Zinduka, MTV Africa Music Awards, Sauti Za Busara, UNAIDS Mkutano wa vijana Mali uliofanyika Bamako, Mkutano wa Kimataifa juu ya VVU na magonjwa ya zinaa ulofanyika Addis Ababa, Ethiopia. Mdee amekuwa akiendesha vipindi kama MTV Base meets, shoo inayolenga kuwawezesha vijana Waafrika kutoka duniani kote kwa kuwapa fursa ya kukaa chini na kiongozi mashuhuri, Kili Music Awards, Epiq Bongo Star Search (EBSS), Dume Challenge, 'Switch On' kampeni ya Airtel, Coke Studio Afrika, Kili Music Tour, Serengeti Fiesta Music Tour, Coca Cola Chart Express, The Hit ya Choice FM, pan-African TV show na MTV Base select 10. Alishawahi kupata tuzo katika Gala mjini New York kutoka kwa UNA-YP, alituzwa na GAVI Alliance kwa msaada wake katika uanzishwaji wa chanjo bure kwa watoto wa Tanzania. Mdee balozi wa GAVI na mpambanaji dhidi ya kansa ya kizazi. Mwaka 2014 alipata mkataba kutoka kampuni ya Crown Paints, kuwa balozi wake nchini Tanzania.

UNAWAZUNGUMZIAJE WADADA HAWA WEMA NA PENNY BAADA YA KUKATAA KUZAA NA DIAMOND>>> NA SASAKUUNDA UKAWA?



Wema Sepetu and Penny Shared these photos on their INSTAGRAM page....is it a real Tabasamu OR Fake



NATEMBEA NA BOSS WANGU, ILA ANATAKA KILA SIKU>>>NAFANYA SANA MAPENZI HADI NIMECHOKA, NISAIDIENI >>>





Mimi Ni Secretary, Natembea Na Boss Wangu, Ila Hanichoki Hata Nikimpa Kila Siku, Jamani Hebu Nisaidieni yani Nafanya Sana Mapenzi Hadi Nimechoka>>>


HII NDIO SEBULE YA ZARI WA DIAMOND>>> SIO KAMA TUNAMSIFIA HEBU JIONEE MWENYEWE






I love MySpace..... it gives me all the peace i need after a long hustling day#HomeSweetHome- Zari wrote this after posting this photo


PICHAZ MTOTO LULU>>>AWAPENDA HATA WANAOMCHUKIA>>>SOMA ALICHOKISEMA




You may not like me but ur following me n my name is in your IG search history......trust me Your a fan....join the Team





JAMANI MASOGANGE MATAMU>>>HEBU JIONEE PICHA ZAKE HIZI AKIWA AMEPANUA MIGUU>>>>NI SHEEDAAHH>>>



  In the name of Instagram, Tanzania socialite, Agnes Masogange shared the photo...HIT or MISS








HIKI NI MOJA YA KITU AMBACHO KINAWATOFAUTISHA ZARI NA WEMA>>>HEBU WACHEKI MARAFIKI WA WEMA NA WA ZARI KISHA UTAPATA JIBU>>>



These are Wema's friends......



Zari's friend



MASHOGA WA AFRIKA MASHARIKI WAFANYA MKUTANO SERENA HOTEL, NI FUL LAANA, JIONEE HAPA






MASHOGA kutoka nchi tatu za Afrika Mashariki wamekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema mashoga hao walikutana juzi katika Ukumbi wa Kivukoni 3 ulioko katika Hoteli ya Serena na kuwashirikisha wasichana wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile. alishuhudia jinsi mkutano huo ulivyokuwa ukiendeshwa kwa usiri wa hali ya juu kwa kuwa kila aliyekuwa akitaka kuingia ukumbini alikuwa akizuiwa.

MITEGO YA BINAMU YANGU JAMANI MMH...YATAKA MOYO...NIMFUNUE AU NIMPOTEZEE...??



 
Mimi na dada yangu mtoto wa mjomba tumekuwa pamoja na kuzoeana sana, hadi wakati mwengine hutaniana kupita kiasi, Binti huyo yani binamu anaishi moshi na mjomba ambako mimi huenda mara kwa mara pindi nikiwa likizo.



Mjomba angu ni mkali sana, na huchunga sana watoto wake wakike, hivyo binamu yangu huyo ni mtoto wa geti kali ile mbaya hakuna kwenda popote zaidi ya kwenye bustani tu iliyopo nje hapo nyumbani.

Mjomba angu huniamini sana hata wakati mwengine husafiri na mke wake na kuniacha nyumbani hapo na binamu yangu huyo. Siku moja mjomba alipata safari ya kwenda nairobi na kuniacha mimi binamu na dada wa kazi. Hiyo siku binti huyo alivaa nguo ambao sijawahi kuona amevaa toka nimjue alikuwa akizunguka hapo ndani huku akijiachia bila wasi wala kujali mimi nipo.

NATAFUTA HATA BOYFRIEND TU JAMANI UPWEKE UNANIUAA, NYEGE NI BALAA



 




Jamani natafuta boyfriend ila awe serious maana huu upweke sasa unaelekea kuniua... Mchumba niliekuwa nae kapata ajali mwaka jana ikiyopoteza maishaa yake... Ni mwaka sasa umepita nadhani nahitaji kurudi sawa Nimechoka kukaa peke yangu upweke noma sana...Nataka mtu Mstaarabu, Mpole kiasi , Mchapa Kazi mwenye Kupenda Maendeleo...

Kama Vipi wacha e-mail yako ama number ya simu...ntaamua yupi nimtafute nijaribu

MWAKA HUO UNAANZA KUSOGEA, UNAENDELEA KUISHI KWENYE PENZI LA GIZA?




WIKI iliyopita tuliianza mada hii ambayo inatufundisha juu ya umuhimu wa kujitambua kupitia makosa tuliyoyapitia, leo tunaimalizia.

Hakuna sababu ya kuishi katika penzi ambalo halina muelekeo mzuri wa baadaye kama ulivyoishi mwaka jana, ni bora kujiengua na kusubiri kumpata yule atakayetambua thamani ya penzi lako na kupanga mipango endelevu.

Kwa wale tuliokuwa pamoja, tuliishia kwenye kipengele cha TATIZO SUGU. Nilieleza namna ambavyo ulikuwa na tatizo sugu mwaka jana, mwaka huu uliepuke.
Endelea...

Ifike wakati uamue moja, tatueni tatizo katika njia stahiki na kama inashindikana basi si vibaya kila mmoja akaanza kuangalia ustarabu mwingine.
Kama mligombana kiasi cha kutosalimiana au kutoheshimiana, mwaka huu uwe na mabadiliko katika tatizo lako sugu, malizana nalo mapema. Usikubali mwaka huu uwe wa majaribio kama ilivyokuwa miaka mingine.
Kama inawezekana, malizeni kikwazo ili muweze kutazama hatua nyingine ya penzi lenu na kama haiwezekani basi bora mkasitisha safari yenu.

WEKENI MALENGO
Kama nilivyotangulia kueleza, hakuna kitu kinachofanikiwa bila ya kukiwekea malengo. Ukishakuwa umetafakari juu ya mtu uliyenaye na kuona ni sahihi au si sahihi basi ni wakati wako sasa kuanza kujiwekea malengo mapya kwa mwaka huu.

Kama uliye naye umeshamtafakari na kuona mnaendana, basi ni vizuri mkaanza kuzungumzia malengo ya penzi lenu. Kama mmeshadumu kwenye uhusiano kwa muda mrefu, jadilini kuhusu ‘future’ ya penzi lenu. Wekeni malengo kwamba, ndani ya mwaka huu lazima tuwe tumefanikisha jambo fulani.
Muweke malengo na myatekeleze kweli. Msikubali yapotelee hewani, tafuteni njia ya kuyafanikisha. Kama ni kuvalishana pete, mvalishane.

Kama ni suala la ndoa basi lazima mjue lina taratibu gani. Mjue njia za kupita ili muweze kutimiza mahitaji yote ya ndoa katika wakati ambao mmejipangia.

FANYA MAAMUZI MAGUMU
Kama uliyenaye unaona hamfanani, haendani na falsafa ya maisha yako, usiogope kuchukua maamuzi magumu. Ni bora ukaamua kuachana naye ili ubaki huru na kusubiri au kutafuta mtu ambaye ni sahihi kwako.
Usikurupuke kumtafuta mwingine. Tafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi. Mshirikishe Mungu katika malengo yako. Muombe akusaidie ili uweze kuyafanikisha. Kama umeamua kwa dhati kutafuta mwenzi wa maisha basi kwa imani yako muombe akuoneshe. Umuone katika macho ya kawaida na hata ya kiroho.

JIFUNZE KUPITIA ULIKOTOKA
Jifunze kupitia aina ya maisha uliyopitia awali. Kama ulikuwa mtu wa kutotulia, jisahihishe na uanze safari mpya. Usijutie kuhusu maisha uliyoyapitia bali angalia kule unapokwenda.
Hakikisha unajipangia mwisho mzuri ili mapito yako yabaki kuwa historia na kuwa somo kwa wengine.

JENGA PICHA YA MBALI
Ili uweze kufikia malengo yako, jenga picha ya mbali na si kutazama karibu. Vuta picha ya ndoa unayotaka kuifunga. Vuta picha ya aina ya familia ambayo unataka kuishi. Jiwekee picha ya familia bora yenye watoto wenye nidhamu, wenye maadili na mtakaoweza kuwasomesha katika shule nzuri.

Ukijiwekea malengo ya mbali na makubwa, hakika utachakarika ili uweze kuyatimiza. Utaweza kujifunza kupitia kwa mifano ya watu mbalimbali waliokutangulia, ukachuja na kupata uelekeo mzuri wa kufanikisha kile ulichokifikiria.

MTITU: SITAKI TENA UONGOZI BONGO MOVIE




Aliyewahi kuwa Katibu wa Klabu ya Bongo Movie, William Mtitu.



ALIYEWAHI kuwa Katibu wa Klabu ya Bongo Movie, William Mtitu amesema inawezekana watu wakawa bado wanahitaji kumuona akiwa kiongozi wa kundi hilo lakini yeye hahitaji tena kuongoza kutokana na kubanwa na kazi zake.

Mtitu ndiye aliyekuwa kiongozi wa kwanza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya mwenyekiti wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kuvuliwa nafasi hiyo kutokana na migogoro ya kimaslahi.

“Nina mambo mengi sana ya kufanya, sina muda wa kuanza kuwania nafasi yoyote pindi itakaporejea tena, kwa sasa nawaachia wale ambao bado hawajashika nafasi hizo,” alisema Mtitu.

Klabu hiyo kwa sasa imepeleka maombi katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ajili ya kupewa usajili wa kudumu kama kundi ikiwa ni pamoja na kupewa kibali maalumu cha kuendesha kazi zao kisheria.

ROSE NDAUKA AFUNGUKA KUTOMMISI MZAZI MWENZAKE



Mwigizaji wa filamu Bongo, Rose Ndauka.


KAMA kawa kama dawa, tunakutana tena katika safu yetu ya Sindano 5, kutokana na maombi mliyonitumia wiki iliyopita tulipoianza safu hii, leo tunawaletea mwigizaji Rose Ndauka ambaye wengi mlimpendekeza awepo katika safu hii.

Mahojiano kati yake na paparazi wetu yalikuwa hivi:
•Paparazi: Rose Ndauka mambo vipi? Siri ya urembo wako ni nini maana kuna tetesi kwamba mkorogo ndiyo unaokufanya uonekane mzuri?
Rose Ndauka: Siri ya urembo wangu anaijua Mungu. Hakuna zaidi ya hapo.

•Paparazi: Umeachana na mzazi mwenzio, Malick Bandawe ambaye mliishi kwa muda mrefu, nini unakimisi kutoka kwake.
Rose Ndauka: Hakuna ninachokimisi kutoka kwake. Maisha yanaendelea!
•Paparazi: Unakumbuka kiasi cha fedha ulichoanza kulipwa katika kazi yako ya kwanza?
Rose Ndauka: Ndiyo nakumbuka, muvi ya kwanza nililipwa laki tatu tu.

Rose Ndauka akiwa na mzazi mwenzake, Malick Bandawe.

•Paparazi: Msanii gani wa kiume unayemkubali sana Bongo Movies?
Rose Ndauka: Kiukweli namkubali sana Single Mtambalike ‘Richie Richie’.

•Paparazi: Wasanii wengi wanapoanza maisha huwa wanapangiwa chumba na wanaume, wewe ulipoanza ulipangiwa na nani?
Rose Ndauka: Sikupangiwa na mwanaume yeyote, nakumbuka kwa mara ya kwanza wakati naanza kupanga nililipa laki moja na ishirini mwenyewe!

Unapenda msanii gani atokee kwenye safu hii? Tuma jina lake kwenda namba 0716-506225.

IYOBO: HATA KAMA AUNT AMENIZIDI UMRI, HAIHUSU




Dansa grade one wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Iyobo akiwa na Aunt Ezekiel.

DANSA grade one wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Iyobo amenyanyua kinywa chake na kusema hata kama mpenzi wake, Aunt Ezekiel amemzidi umri, ataendelea kumpenda hivyohivyo.
Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati, Iyobo.

alisema watu wengi wamekuwa wakihoji yeye kumpenda Aunt
ambaye ana umri wa miaka 29, hawajui tu mapenzi hayaangalii umri kwani miaka ni namba tu za kuhesabika.
“Age is just a number, mimi sioni tatizo kuwa na Aunt. Nategemeaanizalie, awe mama wa watoto wangu. Kuhusu wale wanaosema nina mke mwingine, si kweli yule nilizaa naye tu lakini kwa Aunt ndiyo nimefika,” alisema Iyobo ambaye ana umri wa miaka 23.

LULU: SICHANGANYI MADAWA KAMA WENGINE




Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya sanaa hataweza kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo wasanii wengine wanafanya.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Lulu alisema, amegundua kuwa kila kitu kinatakiwa kifanywe kama kazi na yeye atakuwa akifanya kazi yake ya kuigiza tu na si vinginevyo.

“Napenda kuwa msanii na ninaamini mimi ni msanii, niweke wazi kwamba mimi katika maisha yangu sitarajii kuja kuwa dairekta au script writer wala kuja kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kuigiza.

“Asilimia kubwa ya wasanii hapa kwetu hatuwazi mbali, chochote tunachofanya tunaona ni sawa tu hatupo kibiashara kwa sababu bado ni masikini ndiyo maana wengine wanaigiza ili waonekane, tubadilike,” alisema Lulu.

DAVINA AMPIGIA MAGOTI MAMA KANUMBA




Msanii mkongwe wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’.


MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’, amesema anamuomba radhi mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kwa kutofika kwenye uzinduzi wa kitabu cha marehemu mwanaye kutokana na taarifa hiyo kutomfikia mapema.

Davina alikiri kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao walikuwa karibu sana na marehemu enzi za uhai wake, akasema anaweza kuwa amekosea kwa namna moja au nyingine lakini kikubwa ni kwamba alipata taarifa muda ukiwa tayari umeenda.

“Ni kweli naweza kuchukua lawama kwa upande wangu, namuomba mama yangu anisamehe kwa sababu nilichelewa kupata taarifa nilipompigia Maya kumbe ndiyo muda huo uzinduzi unafanyika,” alisema Davina.
Uzinduzi wa kitabu cha marehemu Kanumba kiitwacho The Great Fallen Tree ulifanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Landmark, Ubungo jijini Dar.

WEMA SEPETU AJUTIA MIMBA YA KANUMBA




Mwanadada asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

Stori: Mwandishi Wetu/Risasi
MWANADADA asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi yao.

Chanzo makini kilicho karibu na Wema kilieleza kwamba, mwanadada huyo kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu huku akijutia mimba aliyopewa na Kanumba ambayo ilichoropoka kwa bahati mbaya na huyo ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito.

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa na marehemu Kanumba.


“Yaani Wema anajutia kweli kwamba kwa nini hakuzaa na Kanumba kwani ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito ambapo kwa sasa anatafuta mtoto lakini hapati, yaani yupo kwenye wakati mgumu sana akikuelezea mwenyewe unaweza kulia kwani ana simulizi ya kusikitisha kuhusu maisha yake na Kanumba.
“Hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa Kanumba anateseka kweli moyoni,” kilisema chanzo hicho.

Alipoulizwa Wema kuhusu ishu hiyo alikiri na kuonesha namna gani anateseka moyoni.
“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena. Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na mimi itatokea nitapata,” alisema Wema.

DIAMOND, ALI KIBA WAKUTANA UKUMBINI, WACHUNIANA!




Duh! Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.

Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye mkutano.

Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar, juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja ya huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya maandalizi ya tamasha.

Waandishi wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya kutaka ‘ubuyu’, hatimaye muda wa kuingia Kiba ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.

Kama ilivyo ada, macho ya waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.

Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya wadau, mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.

Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.

MATONYA AMVAA JAYDEE, KISA PICHA YA UDHALILISHAJI


STAA aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake.

Staa aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’

Akizungumza na mwanahabari wetu, Matonya alisema anamtafuta Jide popote alipo ili amuulize kinaga ubaga kwa nini aliamua kuposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii ikimuonesha akiwa hajitambui pasipo kumtaarifu.

Mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’.

“Nimeumizwa sana na Jide kwa kitendo chake cha kuamua kunidhalilisha kwa kiasi hicho tena akijua mimi ni mwanamuziki mwenzake na kama kuna kitu aliona simfurahishi kwenye mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi kuniita na kunikalisha chini na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye mitandao,” alisema Matonya.

Matonya alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza.



Matonya akiwa mtungi.

“Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani,” alisema Matonya.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.

DAR SASA INATISHA SALUNI YA NGONO YAFUMULIWA



HALI ni mbaya! Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.

Mhudumu wa saluni ya kuchua akitweta mara baada ya kunaswa na OFM akijihusisha na biashara haramu ya ngono.

UCHUNGUZI
Makachero wa kitengo maalum cha Global Publishers cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) walifanya uchunguzi na kugundua kuwa zipo saluni nyingi jijini Dar zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini ndani yake wahudumu wanajiuza hadi miili ambapo wateja wakubwa ni waume za watu na vigogo serikalini.

Kikosi kazi cha OFM kikimtaiti mhudumu huyo.

TUKIO BICHI
Hivi karibuni OFM walipokea simu kutoka kwa mmoja wa wanawake aliyedai kuchoshwa na shughuli zinazofanyika katika saluni moja ya kuchua (massage, jina linahifadhiwa kwa sasa) iliyopo katika eneo la Kinondoni-Morocco, Dar.

Mhudumu huyo mwenye asili ya kisomali akitinga viwalo mara baada ya kunaswa katika mtego wa OFM.

“Jamani nipo hapa nje, nimemfuatilia mume wangu, maana kila siku nasikia huwa anaonekana hapa, hii ni saluni ya kuchua, lakini humo ndani wale wahudumu ni makahaba, wanajiuza tena wanafanyia humohumo ndani, naombeni mje, nataka kufumania,” chanzo chetu kiliongea kwa hasira na uchungu.

...Huyu hapa ndio mhudumu mwenyewe.

OFM MZIGONI
Kama ilivyo kawaida ya OFM kutodharau wito wowote unaohusiana na uvunjaji wa maadili, uonevu na uhalifu, kikosi kilipangwa harakaharaka na kwa kutumia pikipiki ziendazo kasi, zikafika eneo la tukio katika muda muafaka, kwani difenda la polisi, nayo ilionekana ikiingia eneo hilo kuitikia wito wa raia wema.

Baadhi ya vifaa vya kufanyia masaji vikiwa mezani.

KABAAAH!
Ndani ya saluni hiyo, OFM ilishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.

Moja ya vitanda vinavyotumiwa kwa ajili ya biashara ya ngono kwa wateja wanaofika katika saluni hiyo.

Katika chumba cha kwanza, askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa nyama, lakini mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu kilichoashiria kuwa tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, OFM walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.

Mhudumu mwingine aliyenaswa katika saluni hiyo.

WAZINZI WAJITETEA
Baada ya kuwakuta katika hali hiyo, kiongozi wa askari hao, (jina kapuni) aliwauliza kama hiyo ndiyo biashara ya masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini wakabakia kujiumauma pasipo kutoa jibu la kueleweka.
Binti huyo wa Kisomali, ghafla aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai maisha magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo.

Wahudumu walionaswa wakipakizwa kwenye karandinga kuchuliwa hatua za kisheria.

KUMBE ANA MTOTO
Lakini la kushangaza zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa nyumbani alikotoka, ambako ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri wa miezi minne. “Nisameheni jamani, mimi ni mke wa mtu na isitoshe nimeacha kichanga nyumbani, ni shida tu ndiyo imenileta hapa,” alisikika akiomba mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Salma.
Mwanaume aliyekutwa naye, alipoulizwa biashara hiyo inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano yake na mwanamke huyo, ni kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo moja!
OFM iliondoka eneo hilo baada ya askari hao kuwapakiza katika karandinga wanawake wanne na wanaume wawili tayari kwa safari ya kituoni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria

Sunday, 11 January 2015

SAKATA LA IPTL: Mabalozi wamtaka KIKWETE kuchukua hatua kali zaidi...kumtimua tibaijuka haitoshi





Balozi wa Vatican nchini, Francisco Montecillo Padilla (kushoto) akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Mominah wakati wa sherehe za mwaka mpya ziliyoandaliwa kwa ajili ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao na mashirika ya kimataifa.



Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ufafanuzi wa sakata la uchotaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu na kutangaza kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya viongozi na watendaji, nchi wahisani wamesema bado suala hilo linawachanganya na wanasubiri tamko la Serikali.

Nchi hizo, ambazo zilizuia takriban Sh1 trilioni za ufadhili na kuchangia nakisi ya bajeti ya Serikali, juzi zilikiri kuanza kuruhusu sehemu ya fedha hizo baada ya baadhi ya maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuanza kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na kumvua uwaziri Anna Tibaijuka, kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na kumuweka kiporo waziri wake, Sospeter Muhongo na kusababisha Jaji Fredrick Werema kujivua wadhifa wake wa Mwanasheria Mkuu.

Tayari Rais Jakaya Kikwete ameshaeleza kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali.

Hata hivyo, akizungumza juzi, Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini, Timothy Clarke alisema kwamba Serikali imeonyesha jitihada za mwanzo, lakini wanasubiri kuona hatua kali zaidi zikichukuliwa pamoja na kuja na kauli moja kuhusu fedha hizo.

Alisema alichobaini ni kwamba wananchi wengi wanataka kujua hatima ya sakata hilo ndiyo maana walitumia vyombo vya habari kufanya mijadala mbalimbali kuzungumzia wizi wa fedha za escrow ambazo haijawekwa wazi kuwa ni za umma ama ni za Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.

Balozi Clarke alisema kwa upande mwingine, Serikali imeonyesha tabia ya kusita katika kutoa uamuzi kwenye suala hilo na kwamba walitarajia kusikia tamko kali pamoja na tamko la kuzuia vitendo hivyo visiendelee.

Alieleza kuwa hadi sasa nchi nyingi hazijaipa fedha Tanzania kama zilivyokuwa zinatarajiwa kwa kuwa bado zinasubiri hatua zaidi kutoka serikalini.

Sakata la escrow, lililohusu uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka akaunti hiyo, lilisababisha Taasisi ya Marekani ya MCC inayosaidia nchi zinazoendelea, kutangaza kusitisha kusaini mkataba wa awamu ya mpango huo wa maendeleo kuishinikiza Serikali kushughulikia kashfa hiyo.

Bodi ya Wakurugenzi ya MCC ilitoa taarifa yake Desemba 16 mwaka jana, ikieleza kuwa mkutano wake wa Desemba 10 mwaka huu uliruhusu kuanza maandalizi ya kusaini mkataba wa awamu ya pili ya mpango huo, lakini ulielezea hofu na masikitiko kuhusu hali ya rushwa inavyoendelea Tanzania.

Fedha ambazo Tanzania ilipaswa kupata kupitia mradi huo wa MCC awamu ya pili ni Dola 450 milioni ambazo ni sawa na Sh765 bilioni.

“Japokuwa bodi ilipiga kura kwa dhati kabisa ya kuiruhusu Tanzania iendelee na maandalizi kwa ajili ya mkataba wa pili, inaihimiza Serikali ya Tanzania kuchukua hatua thabiti na mahsusi za kukabiliana na rushwa kama sharti la msingi kwa bodi hiyo kufanya uamuzi wa mwisho wa kuidhinisha mkataba huo.
Sakata la escrow lilihusisha fedha zilizokuwa zimehifadhiwa Benki Kuu wakati kesi baina ya Shirika la Umeme (Tanesco) na IPTL zikipambana mahakamani. Pande hizo mbili zilikubaliana kufungua akaunti hiyo ya escrow ili kutunza fedha ambazo Tanesco ilitakiwa iilipe IPTL ikiwa ni malipo ya ununuzi umeme.

Hata hivyo, akaunti hiyo ilifungwa kwa njia ambayo ilitia shaka na fedha hizo kulipwa kwa Kampuni ya Pan African Power Solution Limited (PAP) ambayo ni mmiliki mpya wa IPTL na kukiwa na mambo mengi yaliyotakiwa kufanyiwa kazi kabla ya malipo hayo, ikiwa ni pamoja na kulipwa kwa kodi ya Serikali na kukokotoa upya gharama ambazo Tanesco ilitakiwa ilipe baada ya mzozo wao kuisha mahakamani.

Pia, fedha hizo zililipwa kwa James Rugemarila aliyekuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa za IPTL na ambaye baada ya malipo alitoa mgawo wa fedha kwa watu kadhaa, wakiwamo viongozi wa dini, watumishi wa umma, mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa zamani, hali iliyotia shaka zaidi kuhusu fedha hizo.

Tayari Tibaijuka amewajibishwa baada ya kupokea Sh1.6 bilioni kutoka kwa Rugemarila, hali kadhalika Andrew Chenge, ambaye pia alipewa Sh1.6 bilioni na William Ngeleja (40.4 milioni) wametakiwa kuondolewa kwenye uenyekiti wa Kamati za Bunge sambamba na Victor Mwambalaswa na Fredrick Werema, akitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Mwanasheria Mkuu kwa maelezo kuwa ushauri wake haukueleweka na kuzua tafrani.

Naye Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alisema mazungumzo na Serikali bado yanaendelea na kwamba hali itaendelea kuwa nzuri kadri mazungumzo yanavyoendelea.

“Bado tunaendelea na mazungumzo na Serikali huku tukisubiri tamko,” alisema Dianna.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo wa wahisani, Sinikka Antila juzi ilieleza kuwa mpaka sasa zimekwishatolewa Dola 84 milioni sawa na asilimia 15 ya msaada wote kwenye bajeti ya 2014/2015.

Kwa upande wake, kiongozi wa mabalozi waliopo nchini, Juma Mpango alisema Tanzania imeonyesha jitihada katika kuleta maendeleo na kupambana na rushwa.

Balozi Mpango, ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alisema Serikali imeonyesha nia ya kupunguza matukio ya kifisadi.

“Tumefuatilia namna ambavyo Tanzania imefanya vita kubwa kuondoa madhara ya ufisadi katika nchi, ilikuwa kubwa sana,” alisema Balozi Mpango. Nchi na wadau wanaochangia kwenye bajeti na sekta nyingine za maendeleo ni; Canada, Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Sweden, Uingereza, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jumuiya ya Ulaya (EU) na Benki ya Dunia (WB)