ALIYEWAHI kuwa Katibu wa Klabu ya Bongo Movie, William Mtitu amesema inawezekana watu wakawa bado wanahitaji kumuona akiwa kiongozi wa kundi hilo lakini yeye hahitaji tena kuongoza kutokana na kubanwa na kazi zake.
Mtitu ndiye aliyekuwa kiongozi wa kwanza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya mwenyekiti wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kuvuliwa nafasi hiyo kutokana na migogoro ya kimaslahi.
“Nina mambo mengi sana ya kufanya, sina muda wa kuanza kuwania nafasi yoyote pindi itakaporejea tena, kwa sasa nawaachia wale ambao bado hawajashika nafasi hizo,” alisema Mtitu.
Klabu hiyo kwa sasa imepeleka maombi katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ajili ya kupewa usajili wa kudumu kama kundi ikiwa ni pamoja na kupewa kibali maalumu cha kuendesha kazi zao kisheria.
No comments:
Post a Comment