AZAM TV leo imefunga droo yake iitwayo ‘Mtonyo Chapchap na Azamu TV’ kwa kuwazawadia Watanzania zaidi ya shilingi milioni 15.
Droo hiyo ilianza rasmi Novemba 24 mpaka Desemba 31 mwaka jana, kwa kupata washindi zaidi ya 90 kwa nchi nzima huku washindi wa Dar wapatao kumi na nane baadhi yao wamekabidhiwa pesa hizo na Ofisa Mawasiliano wa Azam TV , Irada Mtonga, na Meneja Masoko, Mgope Kiwanga.Zawadi hizo zimetolewa leo katika ofisi za Azam TV zilizoko eneo la Tazara, Barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment