Thursday, 8 January 2015

DIAMOND NA ZARI SASA NJE NJE, ONA HAPA WAKILANA DENDA HADHARANI BAADA YA SHOO NIGERIA





‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari’ wakifanya yao.

Acha muvi iendelee! Ile projekti ya mastaa wakubwa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari’ sasa imenoga.
Mastaa wakubwa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari’wakila ujana.
Habari zinaeleza kwamba katika pati ya mwaka ya Zari wiki iliyopita iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Guvnor uliopo Kampala, Uganda mwanadada huyo hakuishia kwenye pati tu bali alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Diamond aliyekuwa mgeni rasmi kuwa kwa sasa wao ni wapenzi.
Mbali na mahaba niue waliyooneshana mbele za watu, wawili hao walitumia chansi hiyo ‘kudendeka’ mbele ya kamera hivyo kudhihirisha kwamba mambo yao yapo juu ya mstari.
 

No comments:

Post a Comment