Friday, 9 January 2015

HAYA NDO MAMBO YAKUFANYA WAKATI WA TENDO LA NDOA KUMRITHISHA MPENZI WAKO


Naam wapendwa wa kona yetu ya michano, ningekuwa kwenye gemu la muziki ningejiita mama wa michano yaani muziki wa wagumu, usioogopa mtu yoyote atakayejipendekeza inampa kubwa. Najua kesho ni sikukuu kila mtu amejiandaa kufanya kamamuzi ya kufa mtu au sio jamani?

Utakuta kuna mtu ana ofa zaidi ya kumi na kujiuliza aende ipi na aiache ipi, wapo ambao sikukuu itawaishia vibaya na kujuta kugida vitu vya watu maana vitawatokea puani. Leo nataka kuzungumza na wenzangu na mie, ofa upewe peke yako bila aibu eti unataka kumkomoa buzi unaleta na shoga zako kibaya mpambe anakula kuliko mwenye mali.

Msione wanawake wazuri wakitembea njiani huenda ana mwezi hajanywa hata glasi ya bia, siku akikaribishwa kwenye ofa basi siku hiyo ndo siku ya kumaliza hasira za mwaka mzima.
Mwakwetu lazima tuwe wastaarabu, unapoalikwa au kupewa ofa na buzi unatakiwa uende peke yako, sio uende na wenzako, baada ya kula vya watu utambae taratibu kwa kujifanya umepata dharura. Nani alikuambia dharura inakuja baada ya kula vya watu au umesahau kila mla cha mwenzie na chake huliwa?

Nakumbuka Krismasi moja kuna shoga yangu mmoja alinialika kwa buzi lake, sio kwamba nami sikuwa na buzi bali alipata safari ya ghafla na kuniachia pesa ya kujirusha.

Lakini siku zote raha ya sikukuu kampani basi nilitoka na shosti wangu hadi kwenye hiyo baa moja maarufu jirani na tunapokaa, sehemu walipokubaliana kukutana na buzi lake, tukiwa katika kukata maji si ndio nikapata simu kutoka kwa buzi langu jingine ikabidi niwaache waendelee na raha zao.

Kama ujuavyo nilikwenda anga za kimataifa na buzi langu meneja wa kampuni ya mafuta, tulikula raha zetu kisha nikampa haki yake iliyomkata kiu majira ya saa tano usiku alinirudisha kwangu ili awahi kwake si unajua wanaume za watu pamoja na kugawa raha za wake zao lakini huwa hawalali nje kumfanya mkewe aamini mumewe!

Tukiwa tunakaribia maeneo ya nyumbani gari la mister wangu lilimulika wanaume kama sita wakitaka kumbaka mwanamke si ndiyo akasimama, si unajua tena watu wazito alitoka na ‘mguu wa kuku’ (bastola) ili kumwokoa yule mwanamke ambaye gauni lake lilikuwa limechanika upande.

Wakati akiongea nao si na mimi nikasogea ili nisikie kuna tatizo gani la wale wanaume bila aibu kutaka kumbaka yule mwanamke njiani. He! Kufika ni shoga yangu aliponiona alinirukia na kuning’ang’ania shingoni huku akipiga kelele.

“Anti Na usiniache wataniua hawa kina baba.”
“Unamjua?” Mister wangu aliniuliza.
“Eeh, ndiye aliyenipa ofa mchana baada ya simu yako nikamwacha lakini ajabu si huyu niliyemwacha naye, kwani vipi shosti?” nilimuuliza shoga yangu.
“Baada ya kuondoka wewe na yule mtu wangu alipigiwa simu akaondoka na kuniachia hela ya teksi na bia kumi, lakini kina kaka hawa walikuwa pembeni waliniomba niwape kampani.”
“Sasa tatizo nini?”

“Nimekubaliana na mmoja, wanataka wote.”
“Sikiliza sister kama mtu wenu tupeni chetu muondoke naye,” alilalama mmoja.
“Mnadai shilingi ngapi?”
“Amekula makongoro mawili, nusu kuku, chips mayai mchemsho wa samaki bia nane na mbavu tatu za mbuzi.”

“Toba! Mbona mnamsingizia ana tumbo gani la kula vitu hivyo?” nilihoji nikijua wanamsingizia.
“Muulize mwenyewe,” mmoja wa wale jamaa wenye uchu alisema.
“Eti ni kweli?”

“Kweli, nilikuwanao toka saa tisa, naomba uwalipe nitakulipa nyumbani.”
Mmh, tulitazamana na Mister wangu, tulipiga bei na kukuta elfu 42 ambazo tulimlipia na kuondoka naye. Njia nzima nilijiuliza vitu vyote hivyo alikula akitegemea nini na kama tusingetokea wangemfanya nini.
Si kwamba nilikuwa nahadithia hadithi ya mlafi la hasha, bali kuwataarifu sikukuu inakuja mashosti wenzangu kuweni makini na uchunaji wenu usije ambulia maumivu badala ya raha.

No comments:

Post a Comment