Saturday, 10 January 2015

Kalapina afunguka leo kwenye exclusive interview ya clauz, adai watu wanamtaka agombee ubunge soma story kamili









Msanii wa Hip Hop, Kalapina amedai kuwa watu wengi wanamtaka agombee ubunge. Akizungumza na Clouds FM kwenye kipindi cha Bongo Flava, Kalapina amesema pamoja na hivyo anatarajia kutoa wimbo uitwao ‘Mbunge Mtarajiwa’ aliowashirikisha Professor Jay na Afande Sele.
“Watu wanataka hivyo, wananiita nini? Mbunge mtarajiwa nikipita mtaani. ‘Mbunge Mtarajiwa’ ndo ngoma mpya inayokuja baada ya Good Time,” amesema rapper huyo.
“Ngoma ya ‘Mbunge Mtarajiwa inakuja, ndani kutakuwa na waheshimiwa watarajiwa wenzangu. Humo ndani Afande Sele mbunge mtarajiwa, atakuwemo Professor Jay. Kwahiyo tutakuwa na wabunge watarajiwa wenzangu.”
 

No comments:

Post a Comment