Sunday, 11 January 2015

WADAU WA SOKA KUENDELEA KUPATA HABARI ZA MICHEZO KIGANJANI





Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akiongea na wanahabari kuhusu huduma ya michezo kiganjani .

-Kutokupoteza muda mwingi kutafuta habari
-Ni kupitia Vodacom Tanzania

WADAU wa soka nchini na wateja wa Vodacom Tanzania kwa ujumla wanaendelea kupata habari za soka zinazohusiana na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara(VPL), Ligi Kuu ya Uingereza, na masuala mengine mengi yanayohusiana na burudani kupitia simu zao za mkononi kupitia huduma maalum iliyozinduliwa mwaka jana.

Katika huduma hiyo ambayo inawafanya wateja kupata burudani ili kupata taarifa hizo za michezo na burudani anachotakiwa kufanya mteja ni kutuma neno SPORTS kwenda namba 15778 na hapo mteja atajipatia habari motomoto na burudani kwenye simu yake ya mkononi mahala popote pale aliko.

Akiongea kuhusu huduma hii, Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amewasihi wapenzi wa soka na watanzania kwa ujumla kuitumia huduma hii ambapo itawarahisishia kujipatia habari motomoto za michezo na burudani kwa urahisi bila kupoteza muda mwingi.

“Ni rahisi kupata habari za michezo kwa pamoja kupitia simu yako ya mkononi kupitia huduma hii ukiwa popote pale badala ya kupoteza muda mwingi wa kusubiri kusoma magazeti au kufika nyumbani kusikiliza redio na kuzitafuta kwenye intanent, kwa kujiunga na huduma hii utaona maisha yanakuwa murua na tunawaahidi wateja wetu tutaendelea kuboresha huduma zetu na kuwaletea huduma zilizo bora na zenye manufaa kwao”. Alisema Nkurlu.

Vodacom imekuwa ikiboresha huduma mbalimbali ili ziweze kwenda na wakati na kuwanufaisha na kuwapatia burudani wateja wake ambapo mwaka jana ilizindua huduma ya kipekee ya shinda na kabumbu ambayo iliwawezesha wateja wengi kujishindia zawadi za kila aina ikiwemo fedha taslimu.

Mbali na huduma kama hizo za michezo Vodacom imekuwa ikiandaa promosheni za kubadilisha maisha ya wateja mojawapo ikiwa ni ile ya Timka na bodaboda na Vodacom milionea ambapo washindi waliweza kujishindia pikipiki na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 100.

No comments:

Post a Comment